Mwana Isaka aliona uchungu sana utotoni mwake. Mara nyingi akawa hospitalini. Talasimu hazikumsaidia. Siku moja aliisikia sauti kichwani.

Alinifyatulia Bunduki

Na Isac Nyame, Ghana

"Je, amekufa?" babangu alilia aliponiona nimelala chini nikipigwa na risasi. Babangu alipokuwa akiniona nikisogeza nyasi alidhani nilikuwa mnyama, akasema, "Lazima tumwue mnyama na tumpeleke nyumbani kwa chakula." Akafyatua risasi kadhaa zilizoziingia mwilini mwangu.

Ilinichukua miezi mitatu hospitalini baada ya ajali ile. Siku nyingine nilianguka motoni. Siku hiyo nilitaka niwaonyeshe wenzangu jinsi nilivyoweza kuruka moto mkubwa, lakini nikatumbukia humo. Wakati huo ilikuwa miezi miwili kabla sijaondoka hospitalini. Siku nyingine nilijaribu kutungua papai kutoka kwa kileleni. Nilipofika juu, tawi la mti lilivunjika, hivyo nikaanguka chini. Wakati huo ilikuwa majuma saba kabla sijaweza kutoka hospitalini.

SITAWEZA KUTOKA HAPO NIKIWA HAI

Siku nyingine nilitumbukia katika shimo lenye uchafu na mizoga. Nilipokuwa nikizama nilianza kuwaza ya kwamba sitaweza kutoka hapa nkiwa hai, lakini kulikuwa na mtu aliyenisikia nikipiga yowe naye akaniokoa. Baada ya ajali ile, babangu alinilazimisha nimtafute Imamu mkuu ili amwombe Mungu akomeshe ajali zilizokuwa zikinitokea. Huyo Imamu aliandika maneno kutoka kwa Korani. Kisha akayaosha hayo maneno toka kwa ubao na maji hayo yakaingia kikombe. Akaniambia ninywe yale maji kwa maana yatanisaidia nisiendelee kupata ajali.

Walakini niliendelea kuteseka na ajali zaidi! Lakini siku moja sauti kichwani iliniambia, "Yesu Kristu alikufa ili sisi sote tupate kupokea msaada wa Mungu." Kwa hiyo nilimwomba Mungu, "Nakuombe niokoe na ajali hizo, ninaamini ya kwamba ulimtuma Yesu Kristu afe kwa ajili ya dhambi zetu, ili tuweze kupokea msaada wako." Tangu wakati huo huo sijapata tena ajali za aina yo yote. Najua ya kwamba Mungu alinisamehe makosa yangu yote. Nimepokea karama ya Roho ya Mungu, na Mungu anisaidia katika kila njia. "Umkabidhi Bwana njia yako, pia umtumaini, naye atafanya." Zaburi 37:5.)

back to story index


©copyright SOON Ministries

Contact us