Vijana wengine inchini Tanzania walimsaidia jirani wao. Wakampa chakula na hali kadhalika wamjengea nyumba. Wakaelewa maana ya upendo.Kupenda Jirani
Na Julius A. Mwaipungu Tanzania
Kulikuwa mzee mmoja kijijini mwetu, aliyekuwa kapera. Akawa mbali na ukoo wake naye hakuwa na ndugu wala jirani wa karibu. Akaishi peke yake. Baadaye akaugua na ugonjwa uliomlazimisha hata kujipikia chakula, hivyo alikuwa amelala na njaa. Majirani yake walipomwona hivyo, walianza kumtolea msaada wa chakula kila siku, asubuhi, mchana na jioni.
Ugonjwa wake ukaendelea naye mzee alikuwa na matatizo mengine. Nyumba ambamo alikuwamo akiishi ilikuwa imevunjikavunjika, na kila mvua ikinyesha akalowama. Kunde la vijana wakristu walikuja kumjengea nyumba nyingine. Wakaijenga kwa muda wa siku mbili tu. Mzee hakubidhiwa ile nyumba kwa sababu baada ya kuitumia kwa muda wa mwezi moja tu, alifariki dunia.
Hapo vijana na wazee katika kijiji hicho walishirikiana katika mazishi na matango ya huyo mzee. Majirani na vijana hao watuonyesha upendo kwa sababu walimpenda mzee kama ndugu ya tumbo moja. "Msitende neno lo lote kwa kushindana, wala kwa majivuno: bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine." (Wafilipi 2:3,4.)
©copyright SOON Ministries