Koko toka inchini Gabon alikuwa mtumwa wa pombe hadi mwujizi ulibadilisha maisha yake."MTOTO WA SIKU ZOTE"
Na Koko Hillary, Gabon
Wazazi wangu walikuwa waabudu sanamu ambazo ni utamaduni wa Shetani. Mimi sikumjua Mungu wa kweli. Nilikuwa mnywaji mkuu wa pombe. Rafiki zangu waliniita "Mtoto wa siku zote" kwa sababu nilikunywa tangu tarehe 1 Januari hadi 31 Desemba.
Hii ndivyo nilivyogeuka mtoto wa Mungu. Nilikuwa nikijiandaa kwa safari ya kwenda Jamhuri ya Kongo pamoja na mke wangu kwa sababu alikuwa na tatizo la kuchukua mimba. Sisi wawili tulikuwa tumefikiri kumwona mganga-mchawi kututatua tatizo hilo.
Nikapita kituo cha polisi nipate kibali cha kupita. Hapo nilikutana na Mchungaji wa kanisa fulani aliyezungumza nami habari za Yesu Kristo Mwokozi. Alinisihi tuende kuomba kwake jioni hiyo. Nami nilimwuliza mke wangu kama angekubali tutafute jibu la tatizo letu kwa njia hiyo. Alikubali nasi tukamwendea Mchungaji huyo. Baadaye sisi wawili tumekuwa watoto wa Mungu. Miezi 15 baadaye mke alinizalia mtoto wa kiume, ndiye zawadi ya Bwana. "Ombeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtaona, bisheni nanyi mtafunguliwa" (Mathayo 7:7). Sasa mimi ni mwinjilisti nami ninahubiri Neno la Bwana.
©copyright SOON Ministries