A young girl in Togo was lost fourteen days but with God's help her brother found her.
Mtoto alipotea nchini Togo bali Mungu alimsaidia ndugu yake amkute tena.MTOTO ALIPOTEA!
na Akambi Solomon, Togo
Mimi na rafiki yangu twahudhuria kanisani kwani sisi tu Wakristo. Siku ya Ijumaa fulani tulipokuwa tukishughulika kazini, mtoto wa kike mmoja ambaye amekaa kwenye rafiki yangu alipotea. Tulimtafuta bila mafanikio. Jamaa yake walimtukana rafiki yangu kwa sababu alikaa na huyo binti nyumbani bila kujali maisha yake.
Zilipita siku tisa tangu mtoto huyo alipotea na hadi wakati huo tulikuwa hatujaweza kumkuta. Kwa hivyo tulikuwa tayari kukata tamaa walakini tuliomba Mungu sana. Jamaa hiyo walimtendea vibaya kakaye huyo na mkewe kwani walikosa kumpata mtoto.
Jioni ya siku hiyo ya tisa Mungu alitutia mioyo kwa kusema, "ni baba yupi asiyejali maisha ya wanawe au asiyewasaidia mizigo yao?" Kwa hiyo Neno lake lasema, "Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha." (Mathayo 11:28). Zaidi ya hilo alitukumbusha kusema, "Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye hona; naye abishaye atafunguliwa." (Mathayo 7:7,8).
TULIJITAHIDI SANA
Ndipo tulijitahidi sana katika sala. Siku ya nne ya maombi yetu yaani siku ya kumi na mbili tangu kupotea kwake, kumbe alionekana kwenye mama mmoja mGhana ambaye aliishi mjini Lome. Tuliuona mwujiza mkuu kwa sababu hatukuwa na tumaini kubwa kumpata akiwa hai na salama. Mungu alituonyesha jinsi alivyoshughulika maishani mwetu na hali kadhalika jinsi alivyokuwa tayari kutusaidia katika matatizo yote ya maisha yetu. Asante Mungu.
©copyright SOON Ministries