Joseph was always convicted in his heart of all the bad he did until he found God's answer.
Joseph alihukumiwa moyoni mwake siku zote mpaka alipovumbua jibu la Mungu.

NILIHUKUMIWA MOYONI

na Bulabula Joseph, Jamhuri Kidem. ya Congo

Tangu utoto wangu nilikuwa na hamu ya kutafuta njia ya wokovu na ya uzima kwani niliteseka sana kwa kulemewa na dhambi. Hukumu hiyo iliendelea kunikalia moyoni. Nilijaribu mafunzo ya dini nyingi na kisiasa ya juu kusudi niishi vizuri na wenzangu. Mambo hayo yote hayakunisaidia wala kuniridhisha katika tatizo langu la msingi. Je, nifanyaje na dhambi zangu? Sikujua la kufanya, hivyo nilikaa bila jibu la kufaa nami nikakata tamaa kufanikiwa.

Siku moja niliwakaribisha ndugu na dada fulani Wakristo nyumbani mwangu. Nikawaeleza tatizo langu kuhusu kuhukumiwa moyoni. Mara niliwasikiliza maelezo yao nilivumbua ya kwamba Bwana Yesu alinikomboa katika hali hiyo na maumivu yangu. Nikatambua pia ya kwamba ilinibidi nimpokee Yesu Kristo awe Mwokozi wangu kwani yeye ndiye Njia, Ukweli na Uzima. Hilo lilikuwa jibu la Mungu mwenyewe ndipo nilimgeukia. Yeye pekee aweza kunikomboa toka dhambini na hukumuni. Hivyo nilipopata amani yake ilibubujika na kufurika ndani yangu. Hivyo nilipokea ufumbuzi wa maisha yangu. Nimeokoka na kubatizwa.

back to story index


©copyright SOON Ministries

Contact us